
Rapa wa Kenya, King Kaka, ametangaza kuwa yuko mbioni kuzindua albamu yake mpya na amewahakikishia mashabiki kuwa kazi hiyo itakuwa ya kipekee.
Kupitia Instagram yake, Msanii huyo amesema kuwa wiki ijayo atatoa maelezo ya kina kuhusu albamu hiyo na amesisitiza kuwa mashabiki wataipenda kwa kuwa ameweka moyo na nafsi yake yote katika uundaji wake.
Kwa mujibu wake, wimbo mmoja aliouachia hivi karibuni haukuwemo kwenye orodha ya nyimbo zitakazojumuishwa kwenye albamu hiyo. Alieleza kuwa ulikuwa sehemu ya mchakato wa maandalizi lakini haukuingia kwenye orodha ya mwisho.
Albamu hii mpya inatarajiwa kuendeleza jina la King Kaka kama mmoja wa marapa wenye uwezo mkubwa wa uandishi na ujumbe mzito kwenye muziki, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu mwelekeo mpya wa kazi zake.