
Mwigizaji na mama wa watoto wawili, Jackie Matubia, amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya jina lake kuhusishwa na drama ya kifamilia inayomkumba Ellah Ray, dada yake sosholaiti Amber Ray, na aliyekuwa mchumba wake Steve Odek.
Matubia, amesema hana uhusiano wowote na sakata hilo na ameonya watu wanaomchafulia jina kutumia uvumi mitandaoni. Kupitia Insta Story yake, alikanusha madai hayo akieleza kuwa amechoshwa na tabia ya watu kutumia akaunti feki kumhusisha na kashfa ambazo hazina msingi.
Mrembo hyo alisisitiza kuwa, iwapo watu wanataka kumuhusisha na mambo ya uhusiano, basi angalau wawe na ushahidi wa kweli, kwani kwa sasa wanamtupia lawama zisizomhusu. Kauli yake imeweka bayana msimamo wake wa kutoshirikiana na sakata hilo na kutaka jina lake libaki safi.
Jackie alilazimika kujibu baada ya Ellah Ray kumuanika Steve Odek kwa usaliti na kudai anahusiana na wanawake kadhaa, jina la Matubia likiwemo katika tetesi hizo.