Gossip

VJ Patello Amchana Diana B Baada ya Madai ya Chain Feki

VJ Patello Amchana Diana B Baada ya Madai ya Chain Feki

Mzozo kati ya VJ Patello na Influencer aligeukia muziki Diana B umeendelea kuchukua sura mpya baada ya Patello kujibu vikali madai ya kwamba mikufu yake ya dhahabu ni bandia.

Kupitia Instagram, Patello alimshutumu Diana na mumewe Bahati kwa kushindwa kulipa shilingi milioni moja kwa Harambee Stars, akiongeza kuwa wawili hao hawana uhalali wa kuzungumzia vitu vya thamani.

Ugomvi huo ulianza baada ya Patello kukosoa wimbo mpya wa Diana B uitwao Bibi ya Tajiri, ambapo Diana alisikika akijinadi kuwa ndiye rapa bora nchini Kenya huku akionekana kwenye video akirarua picha za marapa maarufu kama Khaligraph Jones na Nyashinski.

Kitendo hicho kilimkera Patello ambaye alimtolea uvivu kwa kudai kuwa hana heshima kwa wasanii halisi wa hiphop, akamtaka aendelee na masuala ya content creation kwa sababu hajui kurap.

Diana B hakusita kujibu mashambulizi hayo kwa kumdharau Patello, akisema kwa kejeli kwamba ni ajabu mtu mwenye mikufu bandia anathubutu kukosoa kazi ya “Bibi ya Tajiri”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *