Wanariadha wa Kenya walifagia medali zote katika mbio za mwaka huu za nusu marathoni za KGL Millennium mjini Accra, Ghana, na kuweka rekodi mpya katika mbio za wanaume na wanawake.
Katika mbio za wanaume, Gilbert Kiprotich alinyakua taji ya mwaka huu kwa kutumia muda mpya wa saa 1 na sekunde 59, akifuatwa na Alfred Cherono kwa saa 1 dakika 01 na sekunde 04 na Paul Eyanae kwa saa 1 dakika 02 na sekunde 12. Muda huo wa Kiprotich ulivunja rekodi ya awali ya mbio hizo na hivyo akajipatia tuzo ya 900,000 shillings.
Shindano la wanawake lilitawaliwa na Hympha Kiteta mwenye umri wa miaka 20, ambaye alimaliza mbio hizo kwa saa 1 dakika 07 na sekunde 42. Lucy Ndambuki na Eunice Muchiri wakafuatia katika nafasi ya pili na ya tatu na hivyo kuipa Kenya nishani zote za mbio hizo.