Msanii kutoka Kenya VJ Patelo amekanusha vikali tetesi zilizokuwa zikisambazwa mitandaoni kwamba alivamiwa na kuibiwa Chains zake za dhahabu katika eneo la Dandora, Nairobi.
Akijibu madai hayo, Patelo amesema anashangazwa na watu wanaobuni stori za uongo ili kutafuta umaarufu na kufuata vichwa vya habari. Ametoa msimamo wake kwamba hajawahi kuibiwa wala kushambuliwa Dandora, na kwamba ukimya wake mtandaoni ni wa kawaida kutokana na ratiba zake binafsi.
Aidha, amewataka wafuasi wake kupuuza taarifa zisizo na msingi na kuendelea kumuunga mkono katika kazi zake za sanaa.
Uvumi huo ulianza baada ya jamaa mmoja kudai kuwa Patelo alinyang’anywa mali zake, jambo ambalo limepelekea mashabiki wengi kuhoji ni kwa nini hakuwa akiposti kwenye mitandao ya kijamii kwa siku mbili zilizopita.