Sports news

Kenya Yavizia Mataji ya Dunia Tokyo Kwa Uongozi wa Chebet na Kipyegon

Kenya Yavizia Mataji ya Dunia Tokyo Kwa Uongozi wa Chebet na Kipyegon

Macho yote yataelekezwa kwa wanariadha nyota Faith Kipyegon na Beatrice Chebet, wanaoshikilia rekodi za dunia, wakati Mashindano ya Riadha ya Dunia yatakapoanza leo katika Uwanja wa Kitaifa wa Japan, jijini Tokyo.

Mwanariadha Beatrice Chebet, anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 5000 na mita 10,000, atashiriki kwa mara ya kwanza katika mbio za mita 10,000 kwenye mashindano haya, akiwa na azma ya kutwaa mataji mawili ya dunia msimu huu.

Chebet tayari ameonyesha uwezo mkubwa katika majukwaa ya kimataifa, baada ya kunyakua nishani ya fedha na shaba katika mbio za mita 5000 kwenye Mashindano ya Dunia yaliyofanyika Eugene, Marekani (2022) na Budapest, Hungary (2023).

Mwanariadha huyo atawaongoza wenzake wakiwemo Agnes Jebet Ngetich ambaye amekuwa akiandikisha matokeo bora katika mbio za kilomita 10 ambapo aliweka rekodi ya dunia ya dakika 28 na sekunde 46 jijini Valencia, na bingwa wa Afrika Janeth Chepngetich ambaye alishinda mbio za majaribio humu nchini.

Mbio za mita 10,000 kwa wanawake zitaendelea kuwa kivutio kikuu, huku taji la dunia likishikiliwa kwa sasa na Gudaf Tsegay wa Ethiopia, ambaye pia anatarajiwa kutetea ubingwa wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *