
Zaidi ya washiriki 21,000 wamejisajili kufikia sasa kushiriki katika makala ya 22 ya mbio za marathoni za Standard Chartered yatakayoandaliwa tarehe 26 mwezi ujao katika bustani ya Uhuru Gardens jijini Nairrobi.
Mwenyekiti wa Kamati andalizi ya mbio hizo David Mwindi ambaye alikuwa akizungumza wakati wa mbio za maandalizi zilizoandaliwa katika Msitu wa Karura anasema wananuia kusajili washiriki wapatao 30,000. Lampard Mutuku alishinda mbio za kilomita 21 wakati wa mbio hizo za maandalizi yaliyowavutia takriban washiriki 1500.
Mashindano ya kila mwaka ya marathoni ya Stanchart yanadhamiria kukusanya fedha kwa ajili ya talanta za siku zijazo, mpango wa kimataifa unaowawezesha vijana kupitia elimu, kuajiriwa na ujasiriamali.