Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Ruth K, amezua gumzo mitandaoni baada ya kukiri hadharani kuwa ana celebrity crush kwa podcaster maarufu nchini Kenya Oga Obinna.
Akizungumza kwa utani katika mahojiano, Ruth K amesema kuwa amekuwa akimpenda Obinna kwa muda na kwamba anavutiwa na ucheshi wake, sauti yake, na jinsi anavyojiheshimu kwenye kazi zake.
Mrembo huyo ameongeza kwa utani kuwa ikiwa Obinna angeonyesha nia, yuko tayari hata kumzalia mtoto wa kiume, jambo lililowafanya mashabiki wake kupasua kicheko na kuanza kumtag mtandaoni. Ruth K alisema kuwa anasema hayo kwa mzaha lakini hakuficha kuwa anamkubali Obinna kwa moyo wake wote.
Kauli hiyo ilisambaa kwa kasi mitandaoni, huku baadhi ya wafuasi wakimtania kuwa ameamua kuweka wazi hisia zake kwa Oga Obinna huku wakipendekeza wawili hao waingie kwenye mahusiano ya kimapenzi ikizingatiwa kuwa mahusiano ya Ruth K na Baba ya mtoto wake yalivunjika.
Baada ya taarifa hizo kuvuma, Oga Obinna amejibu akifafanua kuwa kauli hiyo ilikuwa ya utani na kwamba hana tatizo lolote na Ruth K. Amesema kuwa anaheshimu kazi anayofanya na anaamini walichosema mashabiki ni sehemu ya burudani tu.