Mwanamuziki wa nyimbo za injili Guardian Angel ametangaza mipango mikubwa ya kujenga kanisa lake kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, akisema ni njia yake ya kumrudishia Mungu shukrani kwa wema wake.
Kupitia ujumbe alioweka mtandaoni, Guardian Angel amesema kuwa Mungu amekuwa mwema kwake kwa namna isiyoelezeka, na kwa sababu hiyo ameamua kujitolea kujenga nyumba ya ibada kama ishara ya shukrani na imani thabiti kwa muumba wake.
Msanii huyo amesisitiza kuwa hatua hiyo siyo ya kibiashara wala mradi wa kutafuta misaada, bali ni jukumu la kiroho alilopokea kwa moyo wa unyenyekevu.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa hahitaji fedha wala michango kutoka kwa mashabiki wake, bali bali anawaomba maombi pekee ili Mungu aendelee kumpa nguvu na mwongozo katika kutimiza azma hiyo.