Sports news

Misri Yaipa Kenya Kipigo cha 2–1 Katika Michuano ya Hoki Afrika

Misri Yaipa Kenya Kipigo cha 2–1 Katika Michuano ya Hoki Afrika

Timu ya taifa ya wanaume ya hoki ya Kenya ilianza kampeni yake ya kuwania Kombe la Afrika kwa kupoteza mabao 2–1 dhidi ya wenyeji Misri katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa jana usiku jijini Ismailia.

Saa chache tuu baada ya wenzao wa kike kuanza mashindano yao kwa ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Nigeria, Wanaume wa Kenya walianza vyema, wakipata bao la kuongoza dakika ya 39 kupitia kwa Bethuel Masambu.

Hata hivyo, dakika tatu baadaye, Ragab Hossam aliwasawazishia Wamisri, kabla ya Ragab Mostafa kufunga bao la ushindi dakika nane baadaye, na kuwapa wenyeji pointi tatu muhimu.

Kenya sasa itakutana na Ghana katika mechi yao ya pili siku ya Jumanne, kabla ya kumenyana na Nigeria na Zambia katika mechi zinazofuata za raundi ya kwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *