Rais wa Shirikisho la Wanamuziki nchini Uganda, Eddy Kenzo, amezua gumzo baada ya kutangaza kuwa wasanii wanaoegemea chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Bobi Wine, hawatakuwa miongoni mwa wanaonufaika na msaada wa kifedha kutoka kwa shirikisho hilo.
Kenzo amesema kuwa licha ya baadhi ya viongozi wa juu wa shirikisho, kama vile Pallaso ambaye ni naibu wake, kuwa wafuasi wa NUP, hawataendelea kupata ufadhili wowote kwa kuwa fedha zinazotumika zinatoka kwa serikali inayoongozwa na chama cha NRM.
Kwa mujibu wake, shughuli za shirikisho zinafadhiliwa na serikali ya NRM na hivyo haitakuwa sahihi kutoa fedha kwa wasanii wanaopinga sera za serikali.
Hata hivyo baadhi ya wasanii wameonyesha kutoridhishwa na kauli ya Kenzo, wakidai kuwa shirikisho hilo la sanaa linapaswa kuwa taasisi huru inayowatumikia wanamuziki wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa