LifeStyle

Eric Omondi Aifariji Familia ya Odinga Kufuatia Kifo cha Raila

Eric Omondi Aifariji Familia ya Odinga Kufuatia Kifo cha Raila

Mchekeshaji maarufu Eric Omondi amejitokeza kuonyesha heshima na kutoa pole kwa familia ya marehemu Raila Odinga kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eric ameposti video akionekana nyumbani kwa familia ya Odinga eneo la Karen, Nairobi, akimfariji Mama Ida Odinga. Katika video hiyo, alionekana akiwa na uso wa huzuni huku akishikana mikono na Mama Ida katika ishara ya faraja.

Eric amesema alimtembelea Mama Ida jana jioni ili kuomboleza pamoja naye na kuwataka Wakenya waendelee kuiweka familia ya Odinga kwenye maombi, akisisitiza kuwa wanahitaji nguvu kubwa katika kipindi hiki kigumu.

Kifo cha Raila kimeendelea kugusa nyoyo za Wakenya kutoka nyanja mbalimbali, huku viongozi, wasanii na wananchi wa kawaida wakiendelea kuonyesha huzuni na kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya Odinga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *