Entertainment

Bahati Atangaza Kuachia Wimbo wa Kuomboleza Raila Odinga

Bahati Atangaza Kuachia Wimbo wa Kuomboleza Raila Odinga

Mwanamuziki kutoka Kenya, Bahati, ametangaza kuwa ataachia wimbo maalum wa kuomboleza kifo cha kiongozi wa ODM, Raila Odinga, mchana wa leo.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Bahati amesema kuwa wimbo huo ni njia yake ya kumuenzi kiongozi huyo ambaye, kwa mujibu wake, amekuwa nguzo muhimu katika siasa za Kenya na amegusa maisha ya wengi. Amesema kifo cha Raila kimeacha pengo kubwa ambalo halitasahaulika.

Bahati anajiunga na wasanii wengine waliotoa nyimbo za kuomboleza, akiwemo Akothee, Prince Indah, na Embarambamba, ambao kwa nyimbo zao wameonyesha upendo na heshima zao kwa marehemu kiongozi huyo.

Ikumbukwe kwamba mwaka wa 2022, wakati wa uchaguzi mkuu, Bahati alikuwa karibu sana na Raila Odinga baada ya kutangaza kugombea ubunge wa Mathare kupitia mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya. Uhusiano wao wa kisiasa na wa kibinadamu ulionekana wazi kupitia matukio waliyoshiriki pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *