Gossip

Mchekeshaji Terence Creative Aomba Radhi Jamii ya Kisii kwa Matamshi ya Chuki 

Mchekeshaji Terence Creative Aomba Radhi Jamii ya Kisii kwa Matamshi ya Chuki 

Mchekeshaji kutoka Kenya Terence Creative amelazimika kuomba radhi jamii ya Kisii baada ya kutoa matamshi yaliyotafsiriwa kuwa ya chuki na kikabila kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Terence alizua mjadala mkali mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe unaodaiwa kumlenga aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i, akionekana kufanya utani kuhusu uwezekano wa kiongozi huyo kushinda urais mwaka 2027.

Chapisho hilo liliwakasirisha baadhi ya wananchi, hususan kutoka jamii ya Kisii, waliolitafsiri kama kejeli na isiyoonyesha heshima kwa jamii nzima pamoja na viongozi wake.

Baada ya wimbi la ukosoaji kuongezeka, mchekeshaji huyo alilazimika kufuta chapisho hilo na kuomba msamaha hadharani kwa jamii ya Kisii, akieleza hakuwa na nia mbaya wala dhamira ya kuudhi jamii ya Kisii.

Terrence amesema kuwa ujumbe huo ulikuwa sehemu ya utani wa kawaida, lakini ukachukuliwa vibaya, akisisitiza kwamba anaipenda na kuithamini jamii hiyo pamoja na viongozi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *