Entertainment

Diamond Platnumz: Kuwa Msanii Nchini Tanzania Ni Kazi Ngumu Sana

Diamond Platnumz: Kuwa Msanii Nchini Tanzania Ni Kazi Ngumu Sana

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake baada ya kukosolewa vikali mitandaoni kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutosimama na wananchi katika kipindi ambacho taifa linakumbwa na machungu ya kisiasa na kijamii.

Kupitia Instastory yake, Diamond ameonekana kujibu wakosoaji wake kwa njia ya mafumbo, akisema kuwa msanii nchini Tanzania ni kazi ngumu sana hasa unapojaribu kudumisha amani na heshima katikati ya misukosuko ya kisiasa.

Kauli yake inakuja wakati mashabiki wake wakionyesha hasira na majonzi, wakimtuhumu kwa kukaa kimya wakati baadhi ya Watanzania wanaomboleza wapendwa wao waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa Oktoba 29 uliokumbwa na utata.

Wapo wanaoamini kuwa Diamond, akiwa msanii mwenye ushawishi mkubwa Afrika Mashariki, anapaswa kutumia sauti yake kutetea wananchi, ilhali wengine wanamtetea wakisema kuwa amechagua ukimya ili kulinda taaluma yake na kuepuka migongano ya kisiasa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *