Entertainment

King Saha Asema Bobi Wine Aliibiwa Ushindi wa Uchaguzi wa 2021 Uganda

King Saha Asema Bobi Wine Aliibiwa Ushindi wa Uchaguzi wa 2021 Uganda

Msanii wa muziki nchini Uganda, King Saha, ameibua tena mjadala kuhusu siasa za nchi hiyo baada ya kudai kuwa Bobi Wine ndiye aliyeibuka mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2021, lakini hakuruhusiwa kuchukua uongozi wa nchi.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni nchini humo, Saha amesema anaamini ushindi wa Bobi Wine uliibiwa, na kwamba wananchi wa Uganda wanajipanga kuhakikisha hali hiyo haijirudii tena katika uchaguzi wa 2026.

Mkali huyo wa ngoma ya Zakayo, amesisitiza kuwa safari ijayo wananchi wako tayari zaidi kurejesha kile walichoamini kilipokonywa kutoka kwao, akionyesha imani kubwa kuwa Bobi Wine ataibuka Rais wa Uganda mwakani.

Kwa muda mrefu, King Saha amekuwa mmoja wa wasanii wanaoonyesha hadharani uungwaji mkono kwa Bobi Wine na harakati za People Power, akitumia jukwaa lake la muziki kuhamasisha vijana kuhusu mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *