Msanii nyota wa R&B kutoka Kenya, Otile Brown, ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo amesema itathibitisha hadhi yake kama mfalme halisi wa muziki Afrika Mashariki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Otile ameshiriki picha ya cover ya EP hiyo aliyoipa jina “The Real King of East Africa”, akieleza kuwa amekuwa akiitayarisha kwa muda mrefu kwa moyo wake wote na sasa muda umefika wa kuiachia rasmi.
Kwa mujibu wa msanii huyo, tarehe 21 Novemba 2025 ni siku ya kihistoria kwa mashabiki wa muziki wa Afrika Mashariki, kwani anaenda kuthibitisha kwa vitendo madai yake ya kuwa “The Real King of East Africa.” kwa kuachia EP yake hiyo.
Ingawa hajaweka wazi orodha ya nyimbo au majina ya wasanii watakaoshirikiana naye kwenye kazi hiyo, mashabiki wake tayari wameonyesha hamasa kubwa mtandaoni, wengi wakisubiri kwa hamu kazi hiyo mpya ambayo inatarajiwa kuwa na ubora wa juu kama ilivyo desturi ya Otile.