Mdau wa masuala ya burudani na matukio, Ciggie Johnson, ameweka wazi kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na Vera Sidika licha ya uvumi ulioenea mitandaoni kuwa anatoka na Socialite huyo wa Kenya.
Kupitia mahojiano maalum na runinga ya NTV, Ciggie amesema kuwa uhusiano wake na Vera umejikita zaidi katika shughuli za kibiashara na sio mapenzi kama wengi wanavyodhani.
Ciggie ambaye amewakosesha usingizi wanawake wengi nchini Kenya kutokana na maisha yake ya kifahari, amefafanua kuwa Vera sio aina ya mwanamke anayemvutia kimapenzi na kwamba tofauti ya umri kati yao inafanya jambo hilo kuwa wazi zaidi.
Ciggie amesema kuwa yeye hupendelea mabinti wadogo kiumri, tofauti na Vera ambaye ni mkubwa zaidi kwake.
Wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja mara kadhaa katika matukio ya burudani, hali iliyochochea tetesi kwamba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.