Sports news

Gor Mahia Yaendelea Kutamba Ligi Kuu Kenya

Gor Mahia Yaendelea Kutamba Ligi Kuu Kenya

Gor Mahia iliendelea kushamiri katika Ligi Kuu ya Soka humu nchini walipomenyana na mabingwa watetezi Kenya Police katika mechi yao ya 7 Jumapili alasiri.

Kogalo ambao mara ya mwisho walipomenyana na Polisi walitoka sare bao moja kwa moja tarehe 22 mwezi Juni mwaka huu walionesha ubabe wao huku wakiongoza kwa mabao mawili kwa nunge  kabla ya mapumziko. Green Army ilifunga mapema dakika ya 2 kupitia kwa Felix Oluoch kabla ya Sharif Musa kuongeza la pili dakika ya 29.

Katika michuano nyigine, KCB iliandikisha sare ya kwanza msimu huu baada ya kutoka sare bao 1-1 na Bandari FC. APS Bomet Fc walitoka sare ya bao 1-1 na Mathare United huku Kakamega Homeboyz wakisajili sare yao ya kwanza msimu huu baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na Murang’a Seal. Shabana ilitwaa ushindi wao wa tatu katika mechi 8 baada ya kuilaza Ulinzi Stars bao moja kwa nunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *