Mtengenezaji maudhui mtandaoni nchini Kenya, Baba Talisha, ameomba msaada wa umma kurejesha iPhone 15 Pro Max na Samsung Galaxy S24 Ultra alizopoteza hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa yake, vifaa hivyo vimebeba kazi muhimu za kibiashara, zikiwemo takribani reels 173 zilizohaririwa na 217 ambazo bado hazijahaririwa kwa brands mbalimbali.
Baba Talisha ametangaza zawadi ya Shilingi 50,000 kwa yeyote atakayesaidia kurejesha vifaa hivyo salama. Amesema kupotea kwa simu hizo kumeathiri pakubwa kazi zake za kila siku, ikiwemo ratiba za kutengeneza maudhui na kuwasilisha kazi kwa wateja
Hata hivyo ametoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa simu hizo kuwasiliana naye mara moja kupitia kurasa zake rasmi mtandaoni ikizingatiwa kuwa taarifa ya uchunguzi wa mwisho wa simu hizo zilionyesha eneo la Jamhuri, jijini Nairobi.