Msanii nyota kutoka Kenya Bien-Aimé Baraza ameibuka mshindi wa kipengele cha Music Influencer of the Year katika tuzo za Pulse Influencer Awards 2025 zilizofanyika jijini Nairobi.
Bien alipata tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki na namna alivyotumia mitandao ya kijamii kueneza kazi zake, kushirikiana na mashabiki, na kukuza taswira ya muziki wa Afrika Mashariki.
Tuzo hizo ambazo hufanyika kila mwaka zilitambua watu mbalimbali waliotoa mchango mkubwa katika sekta tofauti za mitandao ya kijamii na ubunifu. Miongoni mwao ni Judy Nyawira aliyechukua tuzo ya YouTube Influencer of the Year, Mjaka Mfine aliyeibuka TikTok Influencer of the Year, na Amber Ray aliyeshinda kipengele cha Lifestyle Influencer of the Year.
Vilevile, Kalondu Musyimi alitunukiwa kama Media & Blogger Influencer of the Year, DJ Shiti alishinda tuzo ya Most Influential Actor of the Year, huku Dem Wa Facebook akiibuka mshindi wa Facebook Influencer of the Year.