Entertainment

Bien Afunga Rasmi Shindano la “All My Enemies Are Suffering”

Bien Afunga Rasmi Shindano la “All My Enemies Are Suffering”

Msanii nyota kutoka kundi la Sauti Sol, Bien Aime Baraza, amefunga rasmi shindano lake la muziki “All My Enemies Are Suffering Open Verse Challenge”, lililovutia mamia ya washiriki kutoka Kenya na mataifa jirani.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Bien ametangaza kuwa hatua ya kupokea video mpya imekamilika, na sasa timu yake iko katika mchakato wa kuchagua mshindi atakayejinyakulia zawadi ya shilingi 130,000 za Kenya.

Mshindi wa shindano hilo anatarajiwa kutangazwa tarehe 21 Novemba 2025, siku ambayo Bien amesema itakuwa maalum kwa kusherehekea vipaji vipya vya muziki vinavyochipukia nchini Kenya.

Challange hiyo ilizinduliwa mapema mwezi Oktoba kama njia ya kuhamasisha ubunifu miongoni mwa wanamuziki wachanga, ambapo washiriki waliombwa kuongeza mistari yao kwenye kipande cha wimbo maarufu “All My Enemies Are Suffering”..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *