Gossip

Pastor Kanyari Akana Kufahamishwa Kuhusu Ugonjwa wa Betty Bayo

Pastor Kanyari Akana Kufahamishwa Kuhusu Ugonjwa wa Betty Bayo

Mchungaji Victor Kanyari amekanusha madai kwamba aliwahi kufahamishwa kuhusu ugonjwa wa mkewe wa zamani, marehemu Betty Bayo, kabla ya kifo chake.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, amesema taarifa za kifo cha Betty zilimuumiza sana, akieleza kuwa kama angeambiwa mapema kuhusu hali yake, angejitahidi kumsaidia kadri ya uwezo wake.

Kanyari amepuzilia mbali madai kwamba hakumpenda Betty, akisisitiza kuwa alimpenda kwa dhati hata baada ya wao kuachana. Amesema licha ya tofauti zao za kifamilia, alikuwa akimheshimu na kumtambua kama mama wa watoto wake.

Mchungaji huyo amewataka watu kuacha kueneza maneno na mijadala kuhusu marehemu, akisema familia inapaswa kupewa faragha na muda wa kuomboleza kwa utulivu.

Marehemu Betty Bayo alifariki dunia mnamo Novemba 10 katika Hospitali ya Kenyatta, ambako alikuwa akipokea matibabu baada ya kugunduliwa na ugonjwa wa damu aina ya acute myeloid leukaemia, wiki moja tu kabla ya kifo chake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *