Gossip

Pipi Jojo Amshangaza Baba yake Kwa Mtindo wa Kipekee wa Nywele

Pipi Jojo Amshangaza Baba yake Kwa Mtindo wa Kipekee wa Nywele

Msanii chipukizi anayezidi kuibukia kwa kasi, Pipi Jojo, amezua gumzo mtandaoni baada ya kumsuprise baba yake Chief Godlove kwa mtindo mpya wa nywele za rasta uliounganishwa na pipi aina ya lollipop, ubunifu ambao umewastaajabisha wengi.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa mtandaoni, baba yake ameonekana kufurahishwa na ubunifu wa binti yake, na hata kumuuliza kwa utani kama ana kipaji cha ziada cha ubunifu wa mitindo kutokana na ujasiri wake wa kujaribu vitu vipya.

Hatua hii imeongeza mwanga zaidi kwa Pipi Jojo ambaye kwa sasa anazidi kuisukuma kwa nguvu EP yake mpya “I Want Mama Proud.”

Kati ya nyimbo zilizopo kwenye EP hiyo, lead single “Chakacha” imeendelea kufanya vizuri zaidi mtandaoni, ikiwa na zaidi ya watazamaji milioni moja kwenye YouTube ndani ya muda mfupi tangu iachiwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *