Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Burna Boy, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kutoa kauli tata akisema kwamba hakumlazimisha mtu yeyote kuwa shabiki wake na kwamba anawapendelea zaidi mashabiki wenye pesa.
Kupitia Instagram Live, Burna Boy, amesisitiza kuwa hakuna mtu anayelazimishwa kufuatilia muziki wake, huku akiongeza kuwa anathamini mashabiki wanaoonyesha uaminifu kwa kazi yake na wanaoweza kumudu huduma anazotoa kama sehemu ya maisha yao ya burudani.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya msanii huyo kuonekana kwenye video inayosambaa mitandaoni akimtoa nje shabiki aliyekuwa amelala wakati wa moja ya maonesho yake ya moja kwa moja.
Tukio hilo liliibua mijadala mikali, ambapo baadhi ya mashabiki walimkosoa wakisema kitendo hicho kilikuwa cha kudhalilisha.