Msanii wa muziki kutoka Uganda, Gloria Bugie, ameweka wazi msimamo wake kuhusu mahusiano, akisema kwa uthabiti kwamba hatawahi kuchumbiana na mwanaume aliye kwenye ndoa.
Akipiga stori na kituo kimoja cha habari, Gloria amedai kuwa hajawahi kuwa kwenye uhusiano wa aina hiyo, na kwamba anajithamini kiasi cha kutoshiriki mwanaume na mwanamke mwingine.
Amesema kuwa wanaume walio kwenye ndoa wamekuwa wakimtumia ujumbe mara kwa mara kupitia mitandao ya kijamii, lakini hana nia kabisa ya kutoka nao kimapenzi.
Gloria Bugie ameongeza kuwa kwa sasa ameelekeza nguvu na muda wake wote kwenye muziki, na anataka kujenga taswira inayojikita kwenye kazi na si tetesi za mitandaoni.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Chikicha, amesisitiza kwamba maisha anayoyaishi ni matokeo ya kazi yake na sio misaada kutoka kwa mwanaume aliye kwenye ndoa kama inavyodaiwa.
Kauli yake imekuja kufuatia madai yaliyosambaa mitandaoni yakimhusisha na uhusiano na wanaume wa watu kutokana na maisha yake ya kifahari.