Entertainment

Eddy Kenzo Adai Chama cha NUP Kimepoteza Umaarufu Uganda

Eddy Kenzo Adai Chama cha NUP Kimepoteza Umaarufu Uganda

Msanii nyota wa Uganda, Eddy Kenzo, ameibua mjadala mpya baada ya kudai kuwa chama cha National Unity Platform (NUP) kimepoteza umaarufu mkubwa nchini Uganda ikilinganishwa na siku za awali za vuguvugu la People Power.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini humo, msanii huyo ameweka wazi kuwa wanachama wengi wa NUP wanakata tamaa kwa kile alichokitaja kama kukosekana kwa mwelekeo thabiti ndani ya chama. Amesema kuwa hali hiyo imechochea baadhi ya wanachama kujiondoa na kujiunga na makundi mengine ya kisiasa kutokana na kukerwa na mwenendo wa chama.

Kwa mujibu wa Kenzo, vuguvugu lililowahi kushika kasi kubwa nchini Uganda sasa limeporomoka, na anaamini uongozi wa NUP unapaswa kumfikia ili kupata ushauri wa kurejesha tena nguvu na uungwaji mkono wa kitaifa aliohudai aliuchangia kuuanzisha.

Ingawa ameendelea kukosoa chama hicho ambacho kinaongozwa na Bobi Wine, NUP bado kinabaki kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Uganda, wakati taifa hilo likijiandaa kuelekea uchaguzi mkuu wa Januari 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *