Entertainment

Harmonize Adai Diamond Aliwavuruga Wasanii wa Label Yake Kwa Ahadi za Uongo

Harmonize Adai Diamond Aliwavuruga Wasanii wa Label Yake Kwa Ahadi za Uongo

Msanii wa Bongofleva Harmonize ameibua tuhuma nzito dhidi ya Diamond Platnumz, akidai kuwa yeye ndiye chanzo kikuu cha kuvunjika kwa lebo yake ya Konde Gang. Amedai kuwa Diamond alijihusisha moja kwa moja katika kuwavuruga wasanii aliokuwa amewalea, kwa kuwapa ahadi za uongo na kuwashawishi kuondoka kwenye lebo hiyo.

Kulingana na Harmonize, Diamond aliahidi kumfadhili msanii Anjella katika matibabu yake pamoja na kumsaidia kupata kolabo na msanii Zuchu, jambo ambalo lilidaiwa kutumika kama chambo la kumtoa katika mwelekeo wa Konde Gang. Harmonize ameeleza kuwa ahadi hizo hazikuwahi kutimia na zimekuwa sehemu ya mikakati ya kuvuruga uongozi wake ndani ya lebo.

Aidha, Harmonize amedai kuwa Diamond alimlipia Ibraah gharama za mawakili wakati msanii huyo alipotaka kujitoa Konde Gang, hatua ambayo anadai ilibuniwa ili kumvuta Ibraah ajiunge na kambi ya Wasafi au kuipunguzia nguvu lebo yake.

Kwa mujibu wa maelezo yake, hatua hizo zote zimechangia kwa kiasi kikubwa kuyumba kwa lebo ya Konde Gang na kusababisha wasanii wake kukosa uthabiti na mwelekeo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *