Msanii nyota wa Bongo Fleva, Zuchu,ameweka wazi mipango yake mikubwa ya muziki na biashara kwa kipindi kijacho cha mwaka wa 2026 hasa kabla na baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Kupitia Instastory yake, Zuchu amesema kuwa bado ana matoleo mawili ya nyimbo (releases) kabla ya Ramadhan kuanza. Ameeleza kuwa nyimbo hizo ni sehemu ya maandalizi yake ya kuendelea kuwapa mashabiki burudani huku akiimarisha safari yake ya muziki.
Mbali na muziki, Zuchu pia ametangaza kuwa yuko katika hatua za mwisho za kuandaa clothing line yake, ambayo inatarajiwa kuwa tayari kabla au wakati wa Ramadhan. Hatua hiyo inaonesha upanuzi wa chapa (Brand) yake binafsi nje ya muziki na kuingia zaidi katika ulimwengu wa biashara na mitindo.
Baada ya Ramadhan, Zuchu amethibitisha kuwa ataachia albamu yake mpya ya Bongo Fleva, ambayo amesema itakuwa na ladha tofauti na yenye ubora wa kimataifa. Ameongeza kuwa albamu hiyo ni sehemu ya mkakati wake wa kuifikisha muziki wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa.