Entertainment

Asake Atoa Tamko la Huzuni Kufuatia Kifo cha Sha Katika Tamasha la Nyayo Stadium

Asake Atoa Tamko la Huzuni Kufuatia Kifo cha Sha Katika Tamasha la Nyayo Stadium

Msanii wa Afrobeat kutoka Nigeria, Asake, ameeleza masikitiko yake makubwa kufuatia kifo cha Karen Lojore, mwenye umri wa miaka 20, aliyefariki dunia baada ya kukanyagwa wakati wa tamasha alilokuwa akiongoza jijini Nairobi, Kenya.

Kupitia taarifa, Asake amesema tukio hilo limemuumiza sana na kuacha majonzi makubwa kwake binafsi pamoja na timu yake. Amesema moyo wake uko pamoja na familia, marafiki na wapendwa wa marehemu Karen Lojore katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Aidha, ameahidi kushirikiana kikamilifu na juhudi zote za uchunguzi ili kufahamu kilichosababisha tukio hilo la kusikitisha.

Asake pia amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji, akieleza kuwa wote waliohusika na uzembe wa kiusalama wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Kauli hiyo imekuja huku familia na marafiki wa marehemu wakiendelea kuitaka serikali na vyombo husika kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha haki inatendeka.

Tamasha hilo, lililojulikana kama Asake and Gabzy Live in Nairobi, liliandaliwa na kampuni ya Tukutane Entertainment. Waandaaji hao wamesema wanashirikiana kwa karibu na mamlaka husika ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo na mazingira yaliyosababisha msongamano mkubwa wa mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *