Entertainment

Mbosso Awajibu Wanaotilia Shaka Uandishi Wake Baada ya Mafanikio ya 2025

Mbosso Awajibu Wanaotilia Shaka Uandishi Wake Baada ya Mafanikio ya 2025

Msanii wa nyota wa Bongo Fleva Mbosso amewajibu wakosoaji wanaotilia shaka uwezo wake wa kuandika nyimbo baada ya mwaka wa 2025 kumwendea vyema kimuziki kwa kuachia kazi zilizopokelewa vizuri na mashabiki.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Mbosso ameonekana kuchoshwa na madai yanayosambaa mtandaoni kuwa anaandikiwa nyimbo zake, akiorodhesha maneno ambayo yamekuwa yakitumiwa kumdhalilisha kisanii.

Hitmaker huyo wa Pawa, ametaja hoja mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumiwa kumdhalilisha mtandaoni, zikiwemo madai kwamba ana talanta bila juhudi, anasaidiwa na nguvu za kishirikina, anategemea teknolojia ya AI na huwa anaandikiwa nyimbo na watu wengine.

Kauli hiyo imechukuliwa na wengi kama ujumbe mzito kwa wakosoaji wake, hasa ikizingatiwa kuwa Mbosso amekuwa akisifiwa kwa uandishi wenye hisia nzito, mashairi yenye kugusa maisha halisi na uwezo wa kuwasilisha ujumbe kwa sauti ya inayovutia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *