Entertainment

Khaligraph Jones Atangaza Book of Jones Kuwa Albamu Bora Zaidi Kuwahi Kutoka Afrika Mashariki

Khaligraph Jones Atangaza Book of Jones Kuwa Albamu Bora Zaidi Kuwahi Kutoka Afrika Mashariki

Rapa mkali kutoka Kenya Khaligraph Jones ametangaza rasmi kuwa albamu yake Book of Jones ndiyo albamu bora zaidi katika historia ya muziki wa Kenya na Afrika Mashariki, akisisitiza kuwa hakuna mradi wowote kutoka ukanda huo uliowahi kufikia kiwango chake.

Kupitia Instastory yake, Khaligraph amesema Book of Jones imeweka viwango vipya katika ubunifu, ubora wa sauti na ujumbe, akieleza kuwa albamu hiyo imebeba hadithi halisi za maisha, mapambano na mafanikio yake kama msanii aliyepitia changamoto nyingi katika muziki.

Papa Jones ameongeza kuwa mradi huo uliandaliwa kwa umakini mkubwa, kuanzia utunzi wa nyimbo, uzalishaji hadi ushirikiano na wasanii mbalimbali, jambo linaloifanya kujitofautisha na albamu nyingine zilizowahi kutoka katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe Albamu hiyo iliachiwa rasmi mwezi Aprili 2025 ikiwa na jumla ya mikwaju kumi ya moto, akiwashirikisha wasanii kama Nyashinski, Modercai, Dyana Cods, Abbas Kubaff na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *