Gossip

Jacqueline Wolper Asema Amekaa Mwaka Mzima Bila Tendo la Ndoa

Jacqueline Wolper Asema Amekaa Mwaka Mzima Bila Tendo la Ndoa

Staa wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper, amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha ya ndoa yake na mume wake Rich Mitindo

Akipiga stori katika kipindi cha A List Reality Show, Wolper ameushangaza umma kwa kufichua siri ya maisha yake ya unyumba. Wolper amesema bila aibu kuwa yeye na mume wake si watu wa kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

Mwigizaji huyo, amesema kuwa kuna nyakati wao hukaa hadi mwaka mzima bila kushiriki tendo la ndoa, lakini hali hiyo haimaanishi kuwa ndoa yao ina matatizo.

Kauli hiyo imezua mijadala mitandaoni, ambapo baadhi ya watu wamepongeza ujasiri wake wa kuzungumza ukweli wa maisha ya ndoa, huku wengine wakieleza mitazamo tofauti kuhusu umuhimu wa tendo la ndoa katika uhusiano wa kifamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *