Entertainment

Eric Omondi Afunguka Kuhusu Ziara ya IShowSpeed Kenya

Eric Omondi Afunguka Kuhusu Ziara ya IShowSpeed Kenya

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii Eric Omondi ameunga mkono wazo lililotolewa na prankster Vindee la kumualika staa wa mitandao na streamer wa kimataifa IShowSpeed kuzuru maeneo yenye vivutio vya utalii nchini Kenya, hasa Kakamega na Kerio Valley.

Kupitia mitandao ya kijamii, Omondi amesema pendekezo hilo linaweza kuwa njia nzuri ya utalii, na utamaduni wa Kenya kimataifa hasa wakati huu ambapo waandaaji wa maudhui na mastaa nchini humo bado hawajafikia makubaliano ya namna ya kumkaribisha staa huyo kwa njia ya kuvutia.

Prankster Vindee alipendekeza kuwa endapo IShowSpeed atazuru Kenya, apelekwe Kakamega kushuhudia na kushiriki tamaduni ya mapigano ya ng’ombe, maarufu katika eneo hilo, kabla ya kuelekea Kerio Valley kwa burudani ya kuruka miamba (cliff diving).

Kwa mujibu wa Vindee, shughuli hizo zingempa IShowSpeed uzoefu wa kusisimua na ambao haupatikana kwa urahisi katika mataifa mengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *