Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba, amfafanua msimamo wake kuhusu mjadala unaotikisa tasnia ya muziki nchini Tanzania, ambapo baadhi ya mashabiki wameamua kuwakataa wasanii kwa kujihusisha na kampeni za kisiasa, hasa katika uchaguzi uliopita uliokumbwa na utata.
Akizungumza kuhusu hali hiyo, Ali Kiba amesema hakuna mtu aliyefurahia kilichotokea kwenye uchaguzi huo, akibainisha kuwa mazingira yalikuwa magumu kwa kila upande.
Hitmaker huyo wa Sella, amesema wasanii hawakuwa na nia ya kuwaumiza au kuwakwaza mashabiki wao, bali wengi wao walikuwa wanatafuta riziki na fursa za kujiendeleza kimaisha.
Hata hivyo, Ali Kiba amesema mwitikio wa mashabiki umekuwa somo kubwa kwa wasanii, akieleza kuwa ni jambo jema mashabiki kufungua mioyo yao na kusema wazi maneno yote ya chuki na maumivu waliyonayo, badala ya kuyaficha.