Gossip

Mke wa Mkubwa Fella Atishia Kuanika Siri Nzito

Mke wa Mkubwa Fella Atishia Kuanika Siri Nzito

Mke wa meneja maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Mkubwa Fella, amezua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kutoa kauli kali zinazolenga watu anaodai wameanza kumchokonoa na kumshambulia kwa maneno.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sweet Fella amefunguka kwa hasira akisema amekuwa akivumilia kwa muda licha ya kushambuliwa mara kwa mara.

Amesema kuwa alifichua jambo dogo tu na watu wameendelea kumsema kwa zaidi ya wiki moja, akionya kuwa endapo atazungumza tena kwa mara ya pili, basi mambo makubwa yatawekwa wazi na mjadala huo utadumu kwa muda mrefu.

Katika ujumbe wake, amewataka wakosoaji waache kujistukia na wasikilize kwa makini anachokizungumza, akisisitiza kuwa baadhi yao hawataki kusikia ukweli kwa kujifanya masikio yao ni mazito.

Kauli ya Sweet Fella imekuja baada ya baadhi ya watu kumkosoa wakidai alitumia vibaya mchango uliotolewa na Diamond Platnumz kwa kula bata Dubai na kumtelekeza mgonjwa, hatua ambayo ilimpelekea hitmaker huyo wa Sasampa kusitisha msaada wa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *