Entertainment

Eric Omondi azindua rasmi mpango wa Youth 47

Eric Omondi azindua rasmi mpango wa Youth 47

Msanii na mwanaharakati wa kijamii Eric Omondi amezindua rasmi mpango wa Youth 47, hatua aliyotaja kuwa ni mwanzo wa safari kuelekea Kenya mpya inayoongozwa na vijana.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Eric Omondi amesema zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura nchini Kenya ni vijana, hivyo sauti zao lazima zisikike na kuthaminiwa.

Amesema kupitia YOUTH 47, vijana hawatabaki tena kuwa wapiga kura wanaotumiwa wakati wa uchaguzi pekee, bali watakuwa viongozi wanaochukua nafasi za maamuzi katika ngazi zote za uongozi.

Kwa mujibu wake, kaunti zote 47 za Kenya ziliwakilishwa katika uzinduzi huo, ishara ya umoja na dhamira ya kitaifa. Amewatakia heri vijana hao katika safari yao ya uongozi, akisema ana imani kuwa mpango huo utaleta mabadiliko makubwa kwenye masuala ya uongozi nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *