Entertainment

Msanii wa Muziki Nina Roz Ashinda Ubunge Uganda Kupitia NUP

Msanii wa Muziki Nina Roz Ashinda Ubunge Uganda Kupitia NUP

Msanii wa muziki nchini Uganda, Nina Roz , ameibuka mshindi katika uchaguzi wa ubunge wa wanawake wa eneo la Sembabule, baada ya kushinda kiti hicho kupitia chama cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na kiongozi wa upinzani Bobi Wine.

Nina Roz, ambaye ni maarufu pia kwa mchango wake katika tasnia ya muziki, aliwania kiti hicho kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kuwashawishi wapiga kura kwa ujumbe wake wa mabadiliko, uwajibikaji na utetezi wa haki za wanawake na vijana.

Ushindi wake unaonekana kuwa pigo kwa chama cha NRM chake Museveni na ni ishara ya kuongezeka kwa ushawishi wa chama cha NUP, hasa miongoni mwa vijana na wadau wa sanaa nchini Uganda.

Kupitia ushindi huu, Nina Roz anaungana na orodha ya wasanii waliogeukia siasa na kufanikiwa, hatua inayothibitisha kuwa sanaa na siasa vinaweza kushirikiana katika kuleta mabadiliko ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *