Bilionea Chief Godlove amefunguka kuhusu uamuzi wake wa kusafirisha baadhi ya magari yake ya kifahari kutoka Dar es Salaam, Tanzania hadi Nairobi, Kenya.
Kupitia mitandao ya kijamii, Godlove amesema hatua hiyo imechochewa na changamoto ya uhaba wa mafundi wenye ujuzi wa kutosha kuyahudumia magari hayo nchini Tanzania.
Mwanamitandao huyo, amesema kuwa magari yake yanahitaji huduma maalum za kitaalam ambazo hazipatikani kwa urahisi nchini humo. Huduma hizo zinajumuisha uoshaji na marekebisho ya kiufundi (service) yanayohitaji ujuzi wa hali ya juu.
Godlove amesema kuwa atakaporejea Dar es Salaam, atafanya tathmini ya iwapo atanunua magari mengine ya kifahari au ataendelea kutumia yaliyopo.