Gossip

Brown Mauzo Asema Valentines’s Day ni kwa Mabinti walio Chini ya Miaka 25

Brown Mauzo Asema Valentines’s Day ni kwa Mabinti walio Chini ya Miaka 25

Mwanamuziki Brown Mauzo amezua mjadala mkubwa mtandaoni baada ya kudai kidai kuwa Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day), ni maalum kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 25.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Brown Mauzo amesema kuwa wanawake waliovuka umri huo wanapaswa kusubiri Siku ya Wanawake Duniani (Women’s Day) kusherehekea siku hiyo, badala ya kushindana na mabinti wadogo.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kutofurahishwa na kauli ya Mauzo, wakisema ni ya kudhalilisha na kupunguza thamani ya wanawake kulingana na umri.

Wengine wamemshutumu msanii huyo kwa kuendeleza dhana potofu kwamba mapenzi au kuthaminiwa kuna kikomo cha umri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *