Msanii wa muziki wa injili nchini Kenya, Guardian Angel, ameanzisha kampeni maalum ya kuhamasisha mashabiki na jamii kwa ujumla kuhusu athari za unyanyasaji wa mtandaoni (cyber bullying),
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Guardian Angel ametoa wito wa kusitisha kabisa vitendo vya unyanyasaji wa mtandaoni, akieleza kuwa tatizo hilo linaelekea kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zaidi za mtandaoni kwa sasa.
Msanii huyo amebainisha kuwa cyber bullying tayari inaathiri hadi asilimia 53 ya watoto, jambo linalotia wasiwasi mkubwa kwa wazazi na jamii kwa ujumla.
Guardian Angel na mke wake Esther Musila wamekuwa miongoni mwa waathiriwa wakubwa wa cyber bullying, hali iliyowasababishia maumivu ya kihisia kiasi cha kutishia kuchukua hatua za kisheria, ikiwemo kuwafungulia mashitaka wahusika wanaowatusi mtandaoni