Entertainment

Eddy Kenzo Aahidi Kumsapoti Grace Khan Ambaye yuko Rehab

Eddy Kenzo Aahidi Kumsapoti Grace Khan Ambaye yuko Rehab

Mwanamuziki nyota wa Uganda na Rais wa Shirikisho la Wanamuziki Uganda (Uganda National Musicians Federation), Eddy Kenzo, ameahidi kuendelea kumsaidia msanii Grace Khan, ambaye anaripotiwa kurejea tena katika kituo cha tiba ya uraibu wa pombe na dawa za kulevya.

Akizungumza kwenye mahojiano hivi karibuni, Kenzo amesema hajakata tamaa juu ya Grace Khan licha ya changamoto anazopitia za matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe kupita kiasi. Msanii huyo wa wimbo “Sitya Loss” ameeleza kuwa ana mpango wa kushauriana na viongozi wengine wa shirikisho hilo ili kutafuta njia bora ya kumsaidia Grace Khan.

Kwa mujibu wa Kenzo, si mara ya kwanza kwa shirikisho hilo kumsapoti Grace Khan, akisisitiza shirikisho lina wajibu wa kusimama na wasanii wake, hasa wanapopitia nyakati ngumu.

Mapema mwezi Januari, taarifa zilisambaa zikidai kuwa Grace Khan alizuiliwa rehab baada ya kushindwa kulipa ada ya takribani shilingi milioni 5 za Uganda (UGX 5 milioni), fedha ambazo zinaripotiwa kudaiwa na kituo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *