Mwanamitandao kutoka Kenya, Ruth K, amekanusha vikali madai yanayosambaa mitandaoni yanayodai kuwa alimdhuru mwanawe kwa makusudi ili kuvutia hisia za baby daddy wake, Mulamwah, na kupata maudhui ya mitandao ya kijamii.
Kupitia waraka mrefu kwenye Instastory, Ruth K amesema hawezi kamwe kumuumiza mtoto wake kwa sababu yoyote ile, akisisitiza kuwa madai hayo ni ya uongo na yenye lengo la kumchafua jina.
Mrembo huyo, ameongeza kuwa kama mama, usalama na ustawi wa mtoto wake ni jambo la kwanza kwake, na kamwe hawezi kuchezea maisha ya mwanawe kwa maslahi ya umaarufu au mahusiano.
Kauli yake imekuja mara baada ya mfanyakazi wake wa nyumbani kudai kuwa wivu wa mapenzi ulimfanya Ruth K kumdhuru mtoto ili kuvutia hisia za baba wa mtoto wake, Mulamwah. Kwa mujibu wa madai hayo, ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati Mulamwah alikuwa na ukaribu na baby mama wake wa kwanza, Carol Sonnie, hali iliyodaiwa kuchochea wivu na mvutano.