Msanii nyota wa hip-hop kutoka Marekani, Kendrick Lamar, ameendelea kuthibitisha ubora wake katika muziki baada ya kuandika historia mpya kwenye tuzo za Grammy.
Kwenye hafla ya 68 za ugawaji wa tuzo za Grammy iliyofanyika usiku wa kuamkia leo huko Jijini Los Angeles, Lamar alifanikiwa kushinda mataji kadhaa. Miongoni mwa tuzo alizonyakua ni pamoja na Best Rap Album kupitia albamu GNX, Best Rap Performance, Best Rap Song na Best Melodic Rap Performance licha ya ushindani mkali alioupata kutoka kwa mastaa wengine wa dunia.
Kupitia ushindi huo, Kendrick Lamar sasa anatajwa kuwa rapper mwenye tuzo nyingi zaidi za Grammy katika historia, akimpiku Jay-Z aliyekuwa ameshikilia rekodi hiyo kwa tuzo 25.
Lamar ana jumla ya tuzo 26 za Grammy alizokusanya katika maisha yake ya muziki, hatua inayomuweka katika nafasi ya kipekee kwenye historia ya muziki wa hip-hop.