Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Mercy Masika, amekiri kuwa alipitia changamoto kubwa katika mwaka wake wa kwanza wa ndoa, hasa katika suala la kumpikia mume wake, akisema hali hiyo ilikuwa mshtuko kwake mwanzoni.
Akizungumza kuhusu uzoefu huo, Masika amesema alijikuta akishangazwa na kuona mume wake amekaa chini akisubiri apikiwe, jambo ambalo halikuwa rahisi kulielewa kutokana na maisha aliyokuwa amezoea kabla ya ndoa na nafasi yake kama msanii mwenye umaarufu mkubwa.
Mercy Masika amesema kuwa umaarufu na ratiba zake za kazi zilimfanya kuona hali hiyo kama mzigo, lakini baadaye alitambua kuwa ndoa inahitaji kujifunza, kujitoa na kubadilisha mtazamo kuhusu maisha ya ndoa na majukumu yake kama mke.