Entertainment

Trump Achukizwa na Mzaha wa Trevor Noah Grammy

Trump Achukizwa na Mzaha wa Trevor Noah Grammy

Rais wa Marekani Donald Trump ameonyesha kuchukizwa na mzaha uliotolewa na mchekeshaji Trevor Noah wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Grammy zilizofanyika usiku wa kuamkia leo.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump amekanusha madai yaliyoibuliwa na mshereheshaji wa hafla hiyo Trevor Noah aliyefanya mzaha kuwa Rais Trump na aliyekuwa Rais Bill Clinton waliwahi kutumia muda wao katika kisiwa cha Epstein.

Trump amesema hajawahi kwenda katika kisiwa hicho wala sehemu yoyote iliyo karibu nacho. Ameongeza kuwa kabla ya mzaha huo, hajawahi hata kushtumiwa na vyombo vya habari kuhusu madai hayo, akiyataja kuwa ni ya uwongo na yenye lengo la kuharibu sifa yake.

Rais Trump pia amemtaka Trevor Noah kurekebisha kauli yake haraka na kwa usahihi, akionya kuwa yuko tayari kuwashirikisha wanasheria wake. Katika ujumbe wake, Trump amemshambulia Trevor Noah kwa maneno makali na kutishia kumfungulia kesi, akisema atamlazimisha kulipa fidia kubwa ya fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *