Msanii wa filamu Bongo, Wastara, ameshindwa kuficha furaha yake baada ya kupokea zawadi nono ya Siku ya Wapendanao kutoka kwa mume wake, Dudu Baya.
Kwa mujibu wa Wastara, zawadi hiyo imegusa moyo wake kwa namna ya kipekee akisema Dudu ndiye mwanaume aliyemfanya ajisikie kweli kuwa mke wa mtu. Amesema kuwa mapenzi anayoonyeshwa kwa sasa ni yale ambayo kwa muda mrefu alikuwa akisikia tu kutoka kwa watu wengine, lakini hakuwahi kuyapitia binafsi. Pia amedai kuwa katika maisha yake hajawahi kupokea zawadi kutoka kwa mpenzi ndani miaka 40 aliyoishi duniani.
Katika mazungumzo ya simu yaliyosambaa mtandaoni, Dudu amesikika akimwaga maneno matamu ya kimahaba huku akimtaka Wastara atunze maua aliyompa, akisema ni ufunguo wa moyo wake. Akideka kwa sauti ya kimahaba, Wastara ameridhia ombi la Dudu baya, akisema atatunze maua hayo kama anavyoilinda moyo wake.
Dudu Baya alimzawadia mpenzi wake Wastara marashi ya thamani, nguo, viatu, maua pamoja na vitu vingine vya gharama kubwa vilivyomwacha Wastara akishindwa kuficha hisia zake.