Msanii wa muziki nchini Kenya Nadia Mukami amewajibu kwa kejeli walimwengu wanaomtaka apunguze uzito, akisema wazi kuwa hana mpango wowote wa kupunguza uzito kwa sasa hasa baada ya kuongeza makalio.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Nadia amesema kuwa amekuwa akipokea maoni mengi kutoka kwa baadhi ya watu wanaodai mwili wake umebadilika na kumshauri arejee kwenye umbo lake la zamani. Msanii huyo amesema ameridhika kabisa na mwonekano wake wa sasa na haoni sababu ya kubadilika ili kuwafurahisha watu mtandaoni.
Nadia amefafanua kuwa baada ya kupata mtoto, mwili wake ulibadilika kwa njia ya asili na hata kuongeza baadhi ya maungo ya mwili ambayo awali hakuwa nayo. Ametaja hasa makalio kuwa ni miongoni mwa sehemu za mwili zilizoongezeka tofauti na kabla ya kuwa mama, jambo ambalo amesema anayakubali kwa moyo mmoja.