Msanii wa Bongo Fleva Harmonize anadaiwa kukasirishwa na kitendo cha mpenzi wake, Kajala Masanja, kusafiri kwenda Nairobi kwa ajili ya shughuli zake za kikazi.
Kwa mujibu wa Kajala, Harmonize alikuwa tayari amepanga kutoka naye siku hiyo kwa ajili ya matembezi maalum. Hata hivyo, hali ilibadilika ghafla baada ya kugundua kuwa Kajala alikuwa na safari ya kuelekea Kenya, jambo ambalo hakulitarajia.
Kajala amesena kuwa kitendo cha yeye kulala Nairobi ndicho kilichomuudhi zaidi Harmonize, kiasi cha kuonesha wazi hisia za kununa na kutofurahishwa na hali hiyo. Ingawa hakufafanua kwa kina mazungumzo yao ya ndani, amedokeza kuwa hali hiyo ilileta sintofahamu kati yao.
Kauli hiyo imeibua mijadala mitandaoni, huku mashabiki wakitoa maoni tofauti baadhi wakisema ni kawaida kwa wapenzi kukerwa na mabadiliko ya mipango ya ghafla, na wengine wakisisitiza umuhimu wa mawasiliano ya mapema ili kuepusha sintofahamu katika mahusiano