Gossip

Khaligraph Jones Aidharau Orodha ya Shabiki Aliyewataja Wasanii Wanaoweza Kumpa Ushindani

Khaligraph Jones Aidharau Orodha ya Shabiki Aliyewataja Wasanii Wanaoweza Kumpa Ushindani

Staa wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonekana kuidharau orodha iliyotolewa na shabiki mmoja mtandaoni iliyowataja marapa wanaodaiwa wanaweza kumzidi uwezo wa kurap.

Kwenye orodha hiyo, shabiki huyo alitaja majina kadhaa mazito kwenye game ya hip hop nchini humo, akiwemo Octopizzo, Elisha Elai, Timmy Blanco, Twenny Eights, Femi One, Abbas Kubaff pamoja na Nyashinski. Aliwataja pia Chris Kaiga, Rekles na Elsy Wameyo kama wasanii wenye uwezo wa kumfunika OG.

Hata hivyo, Khaligraph ameonekana kutochukulia orodha hiyo kwa uzito. Kupitia majibu yake ya kejeli kwa shabiki, ameonesha kuwa haoni kama listi hiyo ina uzito wowote kwake.

Kwa mzaha, amedai kuwa mtoa orodha alisahau kuwaongeza Stivo Simple Boy, Ngesh pamoja na Diana B, akionyesha wazi kuwa anaichukulia kama mjadala wa mitandaoni usio na athari kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *